akiongea mna mwandishi wetu aliyemhoji bwana Kabwe alikuwa na haya ya kuzungumza..
Mwandishi;Umezipokeaje hizi taarifa za wewe kusimamishwa kazi na Rais baada ya tuhuma zilizotolewa juzi na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndugu Paul makonda?
Kabwe;Mimi sina lolote la kuzungumza kwa sababu maamuzi yamekwishatolewa, ninachosubiri ni uchunguzi ufanywe ili ukweli ubainike.
Mwandishi;Ninachotaka kujua ni wewe unazungumziaje suala hili?
Kabwe;Nimekwishakwambia kwamba sina la kuongea kuhusu hilo na pia sina tatizo lolote na uamuzi huo uchunguzi ufanyike na nina hakika kwamba ukweli utajulikana tu,Kama itabainika nimeonewa je, kuna fidia yoyote ntapewa?