
Alikuwa akizungumza na kipindi cha Enewz kinachorushwa hewani na kituo cha Tv cha EATV alisema yeye anamiliki magari zaidi ya moja hivyo hawezi kuazima gari kwa marafiki zake, na kuongeza kuwa hao wanaosema hivyo ni machizi tu.
Lingine alilogusia ni kuhusu yeye kumtambulisha Mchumba wake ambaye ni msanii mwenzake Naj ,kwamba ameshamtambulisha kwa wazazi wake na ameshamvisha pete ya uchumba.Na kuhusu kuoa baraka alisema hiyo ni mipango ya mungu mwenyewe.