Aliyekuwa waziri mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza Hayati ndg.Edward Moringe Sokoine.
Ni wazi kwamba kila siku zinavyozidi kwenda utendaji wa kazi za Rais John pombe Magufuli unazidi
kupata umaarufu,Umaarufu umeanza kuja hivi karibuni ni baada ya kuanzisha operesheni ya kutumbua majipu yaani kuwawajibisha wafanyakazi wasio waadilifu katika nyazifa zao.
Hali hii inakumbusha enzi zile za utawala wa awamu ya kwanza chini ya waziri mkuu wa nyakati hizo Hayati Ndugu Edward Moringe Sokoine akiwa madarakani katika serikali ya awamu ya kwanza ikiongozwa na Hayati baba wa Taifa JK.Nyerere
Leo ni kumbukumbu ya miaka kadhaa ya kifo cha Waziri mkuu ndugu Edward Moringe Sokoine kufuatia ajali ya gari aliyoipata katika eneo la Wami dakawa mkoani morogoro.
Ni Waziri mkuu ambaye mpaka kesho ataendelea kukumbukwa kwa mambo mabalimbali aliyokuwa akiyapigania,Marehemu Sokoine atakumbukwa kwa mambo mengi yakiwemo ya kupiga vita mambo mbalimbali yakiwemo,wahujumu uchumi,Mafisadi, Wala rushwa,na watumishi wazembe kazini.wakwepa kodi na wengineo.
Leo hii tunamuona Rais john pombe magufuli akiendeleza vita dhidi ya mambo mbalimbali yanayochangia kudidimiza uchumi wa taifa hili la Tanzania,Ni dhahiri anafata nyendo za Hayati Sokoine katika harakati zake za kutumbua majipu serikalini na kwenye sekta mbalimbali za uchumi wa taifa la Tanzania.
Amefanya hayo ni baada ya kuwawajibisha watumishi mbalimbali waliokuwa wakikiuka maadili ya uongozi na kutumia ofisi za umma kwa kujinufaisha wao bila kujali maslahi ya taifa,uchumi na wananchi waliowapa nafasi hizo.