Prince Rogers Nelson enzi za uhai wake.
Mwanamuziki maarufu wa nchini Marekani, Prince Rogers Nelson amefariki dunia jana.Prince aliyekuwa na umri wa miaka 57 amekutwa na mauti jana katika makazi yake yaliyopo Minneapolis nchini Marekani.
Alizaliwa Juni 7, 1958 na kutawala chati za muziki kote duniani katika miaka ya 1970 na 1980 kwa vibao vyake maarufu kama vile ‘I Wanna Be Your Lover’ na ‘Little Red Corvette’.
Prince alibuni chapa yake binafsi ya muziki uliokuwa na sauti na ala za mchanganyiko wa muziki wa Rock, funk na psychedelia.
Muziki wake ulikuwa maarufu sana kiasi kwamba aliwahi kuuza takriban albamu milioni 100 huku
kipaji chake kikimwezesha kutunga, kusanifu, kutayarisha na pia kuimba nyimbo zake mwenyewe.
Baadhi ya vibao vya nguli huyo ni pamoja na While My Guitar Gently Weeps, The Most Beautiful Girl in the World, Do Me, Baby, P Control, If I Was Your Girlfriend, Batdance, Breakfast Can Wait, Partyman, Starfish and Coffee, Soft and Wet, U Got the Look, Thieves in the Temple na vinginevyo vingi
.bofya hapa kuona video ya kifo chake