Habari
 hiyo imeandikwa kufuatia ufafanuzi uliotolewa na Bunge jana kuhusu 
maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) dhidi ya 
utekelezaji wa mkataba wa Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi 
Enterprises Ltd  kuhusu mradi wa utambuzi wa alama za vidole (AFIS) 
(Automated Fingerprint Identification System.)
Ndani
 ya habari hiyo pia, Gazeti hilo limeeleza kuwa kamati ya PAC iliwahi 
kuliandikia Jeshi la Polisi kulitaka liwasilishe mkataba huo mbele ya 
Kamati, jambo ambalo si kweli bali ni upotoshwaji wa makusudi wenye 
lengo la kujenga hisia mbaya kuhusu mwenendo wa shughuli za Bunge mbele 
ya Umma.
Ukweli
 ni kwamba PAC haijawahi kuliandikia jeshi la Polisi kama inavyodaiwa na
 Gazeti hilo. Nukuu ya  maelezo ya PAC katika Hansard kwa Afisa Masuhuli
 kuhusu jambo hilo inasema kama ifuatavyo:
“Kamati
 inamuagiza Afisa Masuhuli kuwasilisha maelezo ya kina kuhusu 
utekelezaji wa Mkataba baina ya Jeshi la Polisi na  Kampuni ya Lugumi 
Enterprises  kuhusu mradi wa AFIS. Maelezo hayo yawasilishwe kwa Ofisi 
ya  Katibu wa Bunge kabla ya Jumatatu tarehe 11 Aprili, 2016”.
Katika
 agizo hilo PAC haikuwa imeandika kwa maandishi kuhusu agizo lake hilo 
hadi tarehe 12 Aprili, 2016 ilipo mweleza Katibu wa Bunge aweze 
kuwasilisha agizo hilo kwa maandishi ili liweze kupata Kinga chini ya 
Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ambapo barua iliandikwa na 
kuwasilishwa kwa Afisa Masuhuli ili kupatiwa maelezo hayo kabla ya 
tarehe 18 Aprili, 2016.
Aidha,
 Mwandishi pia amelituhumu Bunge kuwa lina nia ya kuficha ukweli kuhusu 
jambo hili kwa kusema   taarifa ya ufafanuzi iliyotolewa na Bunge ni “kama
 kufunika kombe mwanaharamu apite kwa kujaribu kupotosha maagizo ya 
yaliyotolewa na kamati ya PAC ambayo inataka kuuona mkataba huo”
Ni
 vyema ikafahamika kuwa si jambo jema kwa mwandishi au chombo chochote 
cha habari kulituhumu Bunge linapotekeleza majukumu yake kwa kuwa Bunge 
linafanya kazi zake kwa kwa kuzingatia kanuni zake za Kudumu ikiwa ni 
pamoja na Sheria.  
Ofisi
 ya Bunge inalisihi Gazeti la Nipashe kuomba radhi kutokana na taarifa 
yake hiyo iliyojaa upotoshwaji mkubwa kwa uzito ule ule au kurekebisha 
taarifa yake kulingana na ukweli ulivyo haraka iwezekanavyo.
Imetolewa na;
Ofisi ya Bunge,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
S.L.P 9133,
DAR ES SALAAM.
16 Aprili, 216.
