Ndugu msomaji wa kila siku wa makala zangu leo ningependa kusema yafuatayo katika makal yangu ya leo inayo husu namna ya kuchagua kitunza ngozi ambacho ni salama kwa afya yako.
ZIFUATAZO NI FIKRA POTOFU KUHUSU NGOZI YAKO NA VIPODOZI
1. Kipodozi ambacho kinachubua ngozi ndicho huitwa kipodozi chennye KEMIKALI. Hii fikra potofu ina angamiza afya za watu ungana name ujue kipodozi kipi ni kemikali na kipi sio cha kemikali.
2. Kupatwa kwa chunusi uso mzima ambazo zinashamiri kila siku kuhusisha vipodozi unavyotumia na hatimaye kubadili vipodozi kila siku. Leo hii utajifunza namna gani sumu katika mfumo wa chakula husababisha chunusi sugu na namna gani ya kuondoa tatizo na kukuepusha hatari ya kubadili vipodozi kila siku.
3. Kubadili vipodozi kila mara kwa dhumuni la kuondoa chunusi sio suluhisho kwa ngozi yako.
KIPODOZI CHA KEMIKALI NI KIPI?
Hiki ni kipodozi ambacho kina kiambata ambacho kinaweza kuathiri afya ya binadamu na kusababisha magonjwa na hatimaye ulemavu wa kiafya. Sio kweli kwamba vipodozi vyenye kemikali ni vile tu vyenye KUCHUBUA NGOZI YAKO bali vipodozi vingi tu vimekuwa vikipewa jina la kibishara kuwa ni vya ASILI na sisi watumiaji hutumia bila kuangalia kuwa vina viambata gani ambavyo haviwezi kudhuru miili yetu.
VIPODOZI VYA ASILI NI VIPI?
Hivi ni vipodozi ambavyo vimetokana na vitu asili ambavyo havina mathara kwa kumtumiaji na haviwezi kubadili utendaji kazi wa mwili pia afya ya mgonjwa. Vinaweza kutokana na mimea,matunda na wanyama pia mazao yatokanayo na wanyama kama asali, mafuta nk
VISABABISHI VYA CHUNUSU SUGU
Ni dhahiri kuwa watu wengi tunajua kuwa chunusi husababishwa na utengenezwaji wa mafuta mengi ya sebum ambayo hutengenezwa na tezi iliyopio chini ya ngozi. Mafuta haya yakizidi kiwango huweza kuziba vitundu vidogo vya ngozi na hatimaye ngozi kutopumua vizuri kwani haitaweza kupitisha jasho ipasavyo na hatimaye kutengeneza mkusanyiko wa uchafu kwenye njia ya jasho. Mkusanyiko huu unaweza kuvamiwa na bacteria na hatimaye usaha kutungwa. Lakini hii sio kisababishi kikubwa cha chunusi sugu kwetu sisi binadamu ingawaje pia ni moja wapo ya kisababishi. Zingatia yafuatayo kama visababishi vikubwa vya chunusi sugu
1. Kuzidi kwa vichocheo vya androgen mwilini. Hivi ni vichocheo vinavyo shughurika na uzazi endapo vinapozidi husababisha utengenezwaji wa mafuta ya sebum kwa wingi. Vichocheo hivi huongezeka hasa wakati wa kubarehe ndio maana wengi chunusi hushamiri sana kipindi hiki. Lakini vichocheo hivi huweza kuvurugwa na utumiaji wa vyakula vyenye sukari sana kama soda, na vyakula vingine vya viwandani kama mikate, sambusa, danati na vingine vingi. Hivyo watu wengi hupatwa na matatizo ya chunusu sugu hasa ndogo ndogo hii ni kutokana na mvurugiko wa vichocheo hivi kutokana na maisha tunayo ishi nayo. Kitendo cha kutibu chunusu kwa kutumia sabuni za kupunguza mafuta ni dhahiri kuwa unaweza kupata nafuu lakini tatizo halitakwisha. Hivyo kuhakikisha kuwa unatibu tatizo la mvurugiko wa vichocheo hivi ndipo suluhisho la chunusu sugu litakuwa limeisha.
2. Kuchafuka kwa mfumo wa chakula kutokana na sumu kama mercury, arsenic na sumu zingine nyingi ambazo huathiri mfumo wa chakula mzima. Pia utumiaji wa vyakula vya ngano vyenye kwani vina protini iitwayo GLUTEN kwani ndio kisababishi kikubwa cha cha mfumo wa chakula kutofanya kazi ipasavyo na hatimaye kuharibu mifumo mingi ya utendaji kazi wa mwili. Hivyo watu wengi ambao hupata chunusi vidogo vidogo kama allergy kisababishi kikubwa ni utumiaji wa vyakula vya ngano vyenye GLUTEN.
3. Utumiaji vyakula vya sukari nyingi kwani ndio kisababishi kikubwa cha kuongezeka kwa sukari mwilini na kusabaisha insulin kuongezeka kwenye mzunguko wa damu. Kuongezeka kwa insulin huharibu vichocheo vingine na hatimaye kusababisha madhara makubwa ya mwili katika ndozi yako. Hapa ndipo utakuta watu wanene kupita kiasi haishiwi na vipele vidogo vidogo usoni hii ni kutokana na kwamba ameanza kupata dalili za mwanza za kisukari aina ya pili kwani ni ishara kuwa insulin haifanyi kazi ipasavyo.
4. Maambukizi kwenye ngozi. Kuna watu ambao imekuwa ni kawaida yao pindi tu wanapopatwa na chunusi huenda madukani kununua cream zenye antibiotics kama TETRACYCLINE CREAM, getriderm Na wengine hukimbilia kununua cream kama SONADEMA na nyinginezo. Unachotakiwa kujua ni kwamba sio kwamba hizi tube ni mbaya la hasha!!! Tube hizi zinashauriwa kutumika pale tu unapokuwa na chunusi zenye kutunga usaha. Hivyo tunakushauri utumie antibiotics cream hizi. Hivyo tufuate mashati ya matumizi ya dawa hizi zenye kemikali tuachane na matumizi mabovu na fikra potofu kila chunusi lazima uende phamarcy.
5. Mchafuko wa damu. Kama wewe huwezi kuondolea mwili sumu zinazo ingia mwilini kupitia ngozi, hewa, chakula mwili utaanza kuzito hizo sumu kupitia ngozi. Hivyo kuchafuka kwa ngozi yako ni dalili moja wapo kuwa umelemewa na sumu nyingi mwilini mwako unatakiwa kuzitoa tu hizo sumu kwa kutumia viondoa sumu yani anti oxidant. Hivyo kitendo cha kubadili vipodozi kila siku kwa dhumuni kuwa vimekukataa ni upotevu wa mali na kudhizidi kuingiza sumu zingine mwilini kupitia ngozi hiyo hiyo.
Basi leo ningependa nizungumzie sumu au kemikali ambazo zipo kwenye vipodozi vyetu vya kila siku na madhara yake. Kwani nimeamua kufanya hili baada ya kugundua kuwa watu hawajui nini hasa ya neon kipodozi chenye kemikali. Wengi wetu wamekuwa wakifikili kuwa kipodozi chenye kemikali ni kile ambacho kinachubua ngozi pekee lakini ukweli utajibiwa na maelezo yafuatayo kwa kina yanayo elezea jinsi vipodozi vingine ambavyo havichubui lakini vimebeba kemikali zinazo hatarisha afya zetu
ZIFUATAZO NI AINA ZA KEMIKALI ZINAZO HATARISHA AFYA ZETU KWENYE VIPODOZI
Vipodozi vyenye kemikali hupimwa ukali wa kemikali iliyomo humo kwa kutumia kipimo kiitwacho ENVIRONMENTAL WORKING GROUP au EWG. Hiki ni kipimo kinacho onesha uwezo wa kemikali kudhuru afya ya binadamu. Hiki kipimo kina madaraja makuu matatu yanayo onesha ukali wa kemikali husika kwenye kipodozi au vyakula kama ifuatavyo
1. EWG 0-2- ina madhara kidogo kwa binadamu
2. EWG 3-6- ina madhara ya kati kwa binadamu
3. EWG 7-10 – Inamadhara makubwa kwa binadamu.
Baada ya kuona madaraja ya kubaini viwango vya madhara vya kemikali mbali mbali kwenye vipodozi kulingana na ENVIRONMENTAL WORKING GROUP. Basi hebu naomba tuongelee kemikali mbali mbali zilizopo kwenye vipodozi vyetu vya kila siku na viwango vyake na madhara yake.
1. 1,4 DIOXINE
Hii ni kemikali amabayo hutumika kupunguza sumu ya kemikali kali ambazo zinatumika kutengeneza vipodozi au bidhaa yoyote kwa matumizi ya ngozi.
Ina kiwango cha EWG cha 8 tafsiri yake ni sumu kali zaidi
MADHARA YAKE
a) Inasababisha kansa yani ni CARCINOGENIC kwani ina uwezo mkubwa wa kubadilisha seli za binadamu na kuwa kansa.
b) Ina ua figo yako yani ni kidney toxicant
c) Ina angamiza mfumo wa fahamu wa binadamu hasa ubongo na kusababisha magonjwa ya kusahau ovyo
d) Ina sababisha magonjwa ya mfumo wa upumuaji kama asthma ya ukubwani kutokana na madhara yake katika mapafu
INAPATIKANA WAPI
Aina hii ya kemikali ipo kwa wingi sana katika SHAMPOO na BODY LOTION tunazo tumia kila siku na kusema kuwa ni alama kwani hazichubui.
SOMA HAYA KUJUA KUWA KIPODOZI HIKI KINA 1,4 DIOXINE
a) Vipodozi vyote vyenye viambata hivi, eth, myreth,oleth,laureth na ceteareth ukiona hivi ujue kuwa hii kemikali ilitumika kuziandaa hizi kwa kuzipunguzia makali ya sumu.
b) Vipodozi vyenye PEG
c) Vipodozi vyenye, polyethylene glycol
d) Vipodozi vyenye, polyoxyethylene na Oxynol
Vipodozi vyote vyenye ingredient kama hizo ujue kuwa zina hii kemikali ambayo hadi sasa inaangamiza dunia kwa kutojua elimu hizi.
2. PARABENS
Hii ni aina ya kemikali ambayo ukichunguza kila vipodozi vina hiki kiini. Ili uweze kuhakikisha ni kuwa chunguza kwa makini vipodozi vyako itaikuta ipo katika mifumo aina kuu nne kama ifuatavyo
a) Methyl parabens: EWG 4
b) Ethyl parabens: EWG 4
c) Propyl parabens :EWG 7
d) Isobutyle parabens: EWG 7
MADHARA YAKE
Kemikali ya PARABEN ina uwezo mkubwa wa kuharibu mfumo wa vichocheo vya mwili yani HORMON. Kwani ndiyo kisababishi kikubwa cha kuvurugika na kuongezeka kwa vichocheo vya kike vya estrogen na kupelekea kuwa na maumivu wakati wa hedhi na matatizo mengine yote wakati wa hedhi. Pia husababisha kutokea kwa vimbe kama uvimbe wa titi na uvimbe kwenye kizazi
INAPATIKANA WAPI?
1. DEODORANT SPRAY
2. MAKE UPS
3. SHAMPOO
4. LOTIONS
5. VIONJO KWENYE VYAKULA VYA VIWANDANI
6. DAWA ZA KEMIKALI
NOTE: Soma kwa makini mafuta yako ujue kuwa kemikali hii haipo kwani ndio suluhisho pekee la kuishi bila magonjwa sugu tafadhari kuhudhuria hospitali sio tiba bali kuepuka vitu kama hivi ndio tiba pekee
3. PHTHALATES
Kuna aina kuu nne kama ifuatavyo
a) Diethylhexyl phthalates EWG10
b) Dibutyl phthalates EWG 10
c) Dimethyl phthalates EWG 4
d) DiEHTYL PHTHALATES EWG 3
MADHARA
Inamaliza nguvu zakiume kwa kupunguza kiwango cha testosterone hormone pia ina punguza kiwango cha mbegu zakiume.
INAPATIKANA KATIKA MAJI YA KEMIKLI YA KUSAFISHIA NGUO,CHOO AU GARI, VIFAA VYA PLASTIC VINGI HUTENGENEZWA KWA HII CHEMIKALI
4. TOLUENE EWG 10
Hii aina ya kemikali hupatikana kwenye rangi mbalimbali za kupakalia majumba na vyombo mbali mbali
MADHARA
Matumizi ya mara kwa mara au kutumia kwa muda mrefu yanaweza kusababisha figo yako kuharibika,ini kuugua na kinga ya mwili kushuka
5. TICLOSAN
Hii kemikali hupatikana kwa wingi sana katika sabuni tunazo ogea kila siku. Hasa sabuni zilizo andikwa ANT BACTERIAL SOAP. Angalia kwa makini.
MADHARA
Huvuruga hormone za kike,figo kufa na magonjwa ya moyo.
ANGALIA KOPO LAKO KWA MAKINI KWANI NINA IMANI KUEPUKANA NA HIVI VITU KUTAPUNGUZA GHARAMA ZAKUONANA NA DAKTARI KILA SIKU,KUPOTEZA MUDA WAKAZI UKIHANGAIKA KUTIBU UGONJWA NA KUPOTEZA NGUVU KAZI YA FAMILIA YAKO.
SOMA KWA MAKINI INGREDIENT ZA MAKOPO YAKO UNAPOSOMA ZINGATIA UJUMBE HUU
“Ushauri wangu ni kwamba tuache kupeperusha bendera ya umagharibi (kuiga tamaduni za kigeni), tudumishe mila zetu ikiwemo kula vyakula vya asili, matatizo haya yatapungua kwa kiasi kikubwa,” DR MERCOLA
Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza alinukuliwa wakati mmoja akisema mamlaka hiyo imepiga marufuku vipodozi vyote vyenye viambata sumu, lakini watu wanaendelea kuvitumia.
“Madhara yake ni makubwa, mwanamke mjamzito ni rahisi kuzaa mtoto taahira, au mimba ikatoka,” alisema huku Daktari wa Magonjwa ya Ngozi wa Kituo cha Afya Centre, Isaack Maro akisema wanawake wanaotumia vipodozi vyenye viambata sumu huathirika kwa kiasi kikubwa bila kujijua.
Alisema madini ya zebaki yanayotumika katika vipodozi vingi hayatoki kwa urahisi mwilini kwani hujazana mwilini kwa muda mrefu na kusababisha maradhi.
VIPODOZI HATARI ZAIDI KWA MTUMIAJI : MISS AFRICA, CITROLIGHT, COCODERM, CAROLIGHT, MAXLIGHT, EXTRA CLAIR, TOP LEMON PLUS, BETA SOL LOTION, LEMONVATE CREAM, JARIBU KWANZA, DIPLOSON, SUPER CLAIR, CLAIR MEN, FAIR AND HANDSOME, BIOCLARE, CAROTONE, MEDICATED FADE CREME, PRINCESS CLAIR, EPIDERM, BETASOL, IVAN HABART na SICAIRE.