Rushwa inahitaji nguvu ya pamoja kuikomesha-Majaliwa | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Sunday, May 15, 2016

Rushwa inahitaji nguvu ya pamoja kuikomesha-Majaliwa


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mkutano wa kimataifa uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani ni kiashiria kwamba tatizo la rushwa ni kubwa sana na linataka juhudi za pamoja kukabiliana nalo.
Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Waziri wa Nchi wa Uingereza anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, Justine Greening walipokutana kwenye mkutano huo uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.
Waziri Mkuu ambaye alihudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais John Magufuli, alimweleza Greening kwamba viongozi wa Serikali wa Awamu ya Tano wameamua kupambana na kila ovu linalotokana na janga la rushwa na pia wameamua kuwajibika na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.
“Sasa hivi nchi yetu ina utamaduni mpya wa kufanya kazi na tumeamua kufanya kazi na siyo tena kwa mazoea, tumeamua kuweka utamaduni mpya wa kupiga vita rushwa ili kuleta uwajibikaji na uwazi miongozi mwa watu wetu,” alisema.
Alipoulizwa ni kitu kimechangia kufanya Tanzania ing’are kimataifa katika vita hii, Waziri Mkuu alijibu kwamba Tanzania imetumia mambo manne ambayo ni kuzuia rushwa isitolewe au kupokewa, kampeni za kuelimisha jamii, kufanya mapitio ya sheria na kuwepo kwa utashi wa kisiasa.
“Serikali inachukua hatua za kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi mwezi Julai mwaka huu,” alisema Waziri Mkuu.
Greening alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na rushwa na kwamba ndiyo maana Tanzania ilipewa mwaliko maalumu wa kushiriki mkutano huo kwa vile baadhi ya mataifa yanaziona juhudi zinazofanywa na Serikali.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us