Baada ya June 2 2016 kambi rasmi ya upinzania bungeni kutoa tamko la kutaka Naibu spika wa Tanzania Dr. Tulia Ackson aondolewe madarakani kwa azimio la kuvunja sheria inayoendesha bunge, leo June 3 2016 Wabunge wa CCM wamepinga shinikizo hilo.
Wakiongea mbele ya Waandishi wa habari Dodoma, Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu), Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Abdallah Possi ambaye amesema..>>’Kitu alichokifanya Naibu spika amefanya kwa mujibu wa kanuni, na kama watu hawakuridhika na maamuzi kanuni zinatoa njia ya wao kuyakatia rufaa ‘
‘Kile ambacho Spika amefanya na hii movie inayoendelea sasa ni vitu viwili tofauti na kwakweli haina maana yoyote zaidi ya sarakasi, kwahiyo alichokifanya Spika ni sahihi kwa asilimia mia‘
Naye Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia ni mbunge wa Muleba hajalikalia kimya hili>>>’Matukio ambayo yanatokea hapa bungeni mimi kwa uzoefu wangu na umri wangu nimeliangalia kwa mtizamo wa kitamaduni na kijinsia ‘
‘Jamii inaona mtu akitolewa nje lakini haioni ule mchakato kwasababu bunge halipo live, jamii ijitambue kwamba tunampinga Tulia Ackson amekosea au kwasababu ni mwanamke kijana. ‘