Jana July 23 2016 Rais John Pombe Magufuli alikabidhiwa rasmi nafasi ya uenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM baada ya kupigiwa kura za ndio 2398 kutoka kwa wanachama wa chama hicho ambapo hakuna kura hata moja ya hapana wala iliyoharibika
Baadhi ya viongozi wakiwemo wa vyama vya upinzania walishiri akiwemo mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema, lakini wapo pia waliotamani kufikisha hisia zao kuhusu tukio hilo na mmojawapo ni mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kupitia account yake ya facebook aliandika maneno haya…
"Napenda kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa Chama chake cha CCM akiwa Mwenyekiti wa Tano chama hicho. CCM imeendelea kudumisha utamaduni wa kukabidhiana Uongozi kila baada ya muda
"Jambo ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya Siasa nchini na barani Afrika. Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa Vyama vya Siasa kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.
"Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais." –Zitto Kabwe