Msichana mwenye umri wa miaka 13 nchini Israel amegundua mfumo wa kuzalisha oxygen angani, Kijana wa Kiyahudu Ma’ariv L’Noar aliripoti siku ya alhamisi, katika mahojiano baina ya wanasayansi kutoka Ramat Hasharon.
Mshindi wa hivi karibuni wa tuzo ya Satellite anaitwa Born, alipata tuzo kutoka Israel Space Agency, Roni Oron kwa kutengeneza BioSat, ambayo ilikuwa inatatua matatizo ya wanaanga kwa kujaribu kuthibitisha kwamba maisha juu ya sayari ya Mars yanawezekana.
Oron anasema satellite yake imejengwa kama Bubble kubwa na upande mmoja ina kioo na nyingine ipo wazi, ambayo inasaidia kupenya kwa jua. Katikati kuna capsule, ambayo italeta utando na hewa inaweza kupenya ila maji hayataweza kupenya.
Ndani yake kuna maji na algae, na nje kutakuwa na carbon dioxide. Kwa kutumia njia ya photosyntesis, satellite hiyo itaweza kuzalisha hewa ya oxygen.
Kutakua na kioo cha ziada katika satellite hiyo ambacho kitasaidia jua kuweza kupenya hadi kwenye capsule, ila sio kwa njia ya radiation, ambayo ina madhara katika algae.
Oron amemwambia Ma’ariv L’Noar juu ya msaada anaopata kwa wazazi wake.
"Baba yangu alikuwa na furaha sana wakati mimi nilivyoanza utafiti," alisema Oron.
"Kutoka kwa mama yake Oron alijifunza maisha ya hekima na ubunifu".