Mwanamume mmoja nchini India inasemekana hakuwa na uwezo kifedha ili kuweza kusafirisha maiti ya mkewe kwa kutumia gari ya kubebea wagonjwa hadi kijijini kwao na hivyo ikambidi kuibeba maiti ya mkewe kwa umbali wa zaidi ya kilomita 12, kutoka hospitali aliyofariki, kwani ilishindwa kumsafirisha kwa gari la kuwabebea wagonjwa hadi kijiji mwake.
Mke wa Dana Mjhi, Amang, mwenye umri wa 42, alilazwa hospitali ya Ulaya, mji wa Bhawanipatna jimbo la Orissa. siku ya Jumanne na alifariki dunia siku inayofata kwani alikua akiugua maradhi ya kifua kikuu. katika Bwana Mahji alisema kijiji chake kilikuwa umbali wa kilomita 60 na hakuwa na uwezo wa kulipa gharama ya usafiri wa gari la kuwabebea wagonjwa.
Bwana Mahji, ilimbidi achukue maiti hiyo kwani kwa madai yake wahuduhu walimsihi kufanya hivyo, na alipowaomba wamsadie gari ya kubebea maiti hakuweza kupata ndipo uamuzi wa kumbeba mkewe begani na kuanza safari kuelekea kijijini Melghar kufuata mila na tamanduni za mwisho huku akiungana na mwanawe mwenye umri wa miaka 12
Alitembea kwa takriban kilomita 12, ndipo watu walipoingilia kati na wakaamua kumsaidia gari la kubebea wagonjwa mpaka wakamfikisha hadi mwisho wa safari yake ambako shughuli ya kuchoma mwili wa mkewe ilifanyika siku ya Jumatano usiku.