Serikali imesema imejipanga vilivyo kuhakikisha inawalinda raia na mali zao na kwamba watakao bainika kujihusisha ama kuunga mkono vitendo vya uhalifu ukiwemo ujambazi pamoja na kulibeza jeshi la polisi, watachukuliwa hatua kali.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na maafisa wa jeshi la polisi ,uhamiaji,magereza na vyombo vingine vya ulinzi na usalama usalama,katika mkutano uliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya polisi Moshi mkoani Kilimanjaro nakusema kuwa serikali haita fumbia macho uhalifu
Aidha Waziri Nchemba amelipongeza jeshi la polisi kwa kufanya kazi kwa weledi huku akilitaka lishirikiane na jamii kuzidisha juhudi za ulinzi kwenye maeneo ya pipakai, ili kuthibiti mtandao wa wahamiaji haramu ,magendo ,pamoja na ule wa uingizaji wa madawa ya kulevya nchini .
Pia Waziri Nchemba,katoa angalizo kwa vyombo vya ulinzi na usalama kushiriki vilivyo katika kufanikisha zoezi la uandikishaji vitambuklisha vya uraia