Katika hali isiyokuwa ya kawaida mgahawa mmoja jijini London Uingereza umechukua chati ya aina yake kwakuwa na huduma ya kipekee ambapo wateja wake hula vyakula mbalimbali wakiwa utupu.
Mradi wa kujenga Mgahawa huo wa Bunyadi ulitangazwa na kampuni ya Lollipop Aprili 19 mwaka 2016 na kufunguliwa rasmi tarehe 11 Juni 2016 chini ya mwanzilishi wake Seb Lyall pamoja na timu yake.
Mgahawa huo wa Bunyadi upo kusini mwa mji wa London katika vitongoji vya Elephant na Castle ,una uwezo wa kupokea wateja takribani 42 kwa wakati mmoja na hadi sasa taarifa kutoka mji huo zinasema kuwa takribani watu 42,000 tayari wameweka oda ya kula katika mgahawa huo.
“Naamini kuwa watu wanahaki ya kupata nafasi ya kufurahi bila vizuizi vyovyote kama rangi bandia, umeme, kemikali, simu za mkononi, na hata nguo kama wakitaka,wazo langu kuu ni ukombozi wa kweli” Alisema Lyall
Lyall pia anahusika na bar mbili za Owl Bar na Shoreditch’s Breaking Bad cocktail bar zenye utata mkubwa jijini London.Kampuni yake pia inajulikana kwa kuwa nyuma ya ugunduzi wa programu za simu kama Locappy na Hoot London ambazo ni maarufu sana katika jiji la London.