
Katika
ligi ya mabingwa barani ulaya Bingwa mtetezi wa ligi ya mabingwa barani
ulaya FC BARCELONA ameungana na timu nyingine SABA kufuzu kwa hatua ya
robo fainali ya michuano hiyo
Katika ligi ya mabingwa barani ulaya Bingwa mtetezi wa ligi
ya mabingwa barani ulaya FC BARCELONA ameungana na timu nyingine SABA
kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kupata
ushindi wa magoli MATATU kwa MOJA dhidi ya ARSENAL.
Mabao ya NEYMAR, LUIS SUAREZ na LIONEL MESSI yametosha kuivusha FC
BARCELONA katika hatua ya robo fainali kwa ushindi wa jumla ya magoli
MATANO kwa MOJA dhidi ya ARSENAL.
Bao pekee la kufuta machozi kwa ARSENAL katika mchezo wa jana
uliofanyika nyumbani kwa FC BARCELONA, CAMP NOU limefungwa na kiungo
MOHAMED ELNENY.