Wakati KOREA KASKAZINI, ikiwa imemfunga, miaka kumi na mitano jela pamoja na kazi ngumu, mwanafunzi mmoja raia wa MAREKANI
MAREKANI imeiwekea vikwazo vipya KOREA YA KASKAZINI, ikiwa ni hatua ya kupinga kitendo cha nchi hiyo kumfunga raia wake huyo, ambaye alikwenda KOREA YA KASKAZINI, na kundi la wanafunzi wenzake kwa ajili ya masomo ya kujifunza kwa kutalii.
Mwanafunzi huyo alilazimishwa kuomba radhi hadharani, mbele ya waandishi wa habari. MAREKANI imesema, kitendo kilichofanywa na KOREA KASKAZINI hakiwezu kukubalika na nchi yoyote, kwani kosa alilofanya mwanafunzi huyo, halistahili adhabu kali aliyopewa.
Vikwazo vya sasa vya MAREKANI dhidi ya KOREA KASKAZINI vinawahusu viongozi wa ngazi za juu wa nchi hiyo.