Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela na Katibu Tawala wa Mkoa
huo Abdul Rashid Dachi, kufuatia mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi
kuwa
hauna watumishi hewa.
hauna watumishi hewa.
Rais
Magufuli ametangaza kutengua uteuzi wa Viongozi hao wa Mkoa wa Shinyanga
leo April 11 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, mara baada ya kupokea
Taarifa ya Mwaka 2014/2015 ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU), na kupokea hundi kifani ya shilingi Bilioni 6 kutoka Ofisi
ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotokana na kubana
matumizi.
Rais
Magufuli ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa kuwa Mkoa wa Shinyanga
hauna watumishi hewa, aliamua kutuma timu ya ukaguzi iliyokwenda kufanya
uchunguzi ambapo hadi kufikia jana Aprili, 10 2016 imebaini kuwepo
watumishi hewa 45 huku zoezi likiwa linaendelea katika wilaya mbili za
Ushetu na Shinyanga Vijijini.
>>>’Na
wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi
hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza
sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa
masikitiko makubwa, kwa nini Mkuu wa Mkoa alisema hakuna mtumishi
hewa?’:-Rais Magufuli
Rais Magufuli amesema baada ya kutengua uteuzi wake, Anne Kilango Malecela atapangiwa kazi nyingine.
Pamoja na hatua hiyo, Rais Magufuli ametaka wakuu wa mikoa yote wawafichue watumishi hewa wote ili waondolewe mara moja, na ameagiza timu iliyofanya uchunguzi Mkoani Shinyanga itumike kufanya uchunguzi katika mikoa mingine kwa lengo la kukomesha upotevu mkubwa wa fedha za umma.
Pamoja na hatua hiyo, Rais Magufuli ametaka wakuu wa mikoa yote wawafichue watumishi hewa wote ili waondolewe mara moja, na ameagiza timu iliyofanya uchunguzi Mkoani Shinyanga itumike kufanya uchunguzi katika mikoa mingine kwa lengo la kukomesha upotevu mkubwa wa fedha za umma.
Katikati
ya Mwezi Machi, 2016 Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa yote nchini
kusimamia zoezi la kuwaondoa watumishi hewa wote katika orodha ya
malipo ya mshahara, ambapo mpaka tarehe 31 Machi, 2016 Jumla watumishi
hewa 5,507 walibanika.
Kati ya
shilingi Bilioni 583 ambazo serikali imekuwa ikitumia kila mwezi kwa
ajili kulipa mishahara, kati ya shilingi Bilioni 53 na 54 zimekuwa
zikipotea kutokana na kulipa mishahara ya watumishi hewa.