Gmail sasa itakupa taadhari endapo serikali itakuwa inakuwinda. Hii ni mojawapo ya mwendelezo wa juhudi za kuhamasisha matumizi huru ya mitandao ambayo makampuni mengi makubwa kama Apple imekuwa ikiwekea mkazo.
Gmail sasa inaimarisha ulinzi kwa kukueleza nini kinaendelea kwenye akaunti yako ya barua pepe. Gmail inatanua uwezo wa “safe browsing notifications” ya akaunti yako pale ambapo unataka kufungua uzi (link) ambayo ina mashaka kutoka kwenye barua pepe yako ,gmail itatoa onyo/tahadhari kubwa juu ya link hiyo,
lakini pia kabla link hiyo haijafunguka gmail itakupa tena uamuzi wa kuacha link hiyo na kurudi nyuma iwapo tayari ulishaifungua kwa bahati mbaya.!! Hii itasaidia sana watumiaji kutofungua link zitakazosababisha matatizo/matumizi mabaya ya mitandayo kinyume na matakwa ya mtumiaji binafsi.
Aidha gmail inaendelea kupigania haki za watumiaji wake kwa kutoa taadhari ukurasa mzima endapo inahisi unawindwa na wadukuaji (hackers) wa serikali. Google pia imesema kuwa si zaidi ya 0.1% ya watumiaji wake ndo watakaopokea onyo hili maalumu la ukurasa mzima, hii ni kuwalinda waandishi wa habari na wanaharakati ambao mara nyingi husakwa na serikali zao.