Leo tarehe 19 April 2016 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli amefungua daraja la Kigamboni, daraja la kwanza la kuning’inia (Suspension Bridge) katika Afrika Mashariki likiwa na urefu wa mita 680.
Daraja hilo linaloshika nafasi ya tatu kwa urefu ukiacha daraja la Mkapa linaloshika nafasi ya kwanza (kilomita 1) huku lile la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji (mita 720) lilojengwa kwa ushirikiano kati ya serikali na NSSF, limetumia teknolojia ya kisasa inayotumika kutengeneza madaraja marefu duniani.
Tuanze na kuelewa maana ya Suspension Bridge (Daraja linaloning’inia), hii ni aina ya madaraja inayotegemea kamba, nyaya au vyuma vilivyoungwa katika nguzo kuu za daraja ambazo zinabeba uzito wote wa daraja na vifaa vinavyopita juu yake. Kwa maana nyingine madaraja haya huwa yategemea sana zile kamba zinazoshikiliwa katika nguzo kubeba uzito wa daraja zima. Mfano mzuri katika daraja la Kigamboni kuna nguzo kuu mbili zinazobeba uzito wote wa daraja huku kukiwa na vipande tisa (9) vya chuma kila upande wa nguzo kubeba uzito wa daraja na kuuelekezea katika nguzo.
Faida za madaraja ya kuning’inia (Suspension Bridge)
Uwezo wa kutengeneza madaraja marefu zaidi ukilinganisha na aina ya madaraja mengine
Kiwango kidogo cha material kinachohitajika katika utengenezaji ukilinganisha na aina nyingine za madaraja
Kiasi kidogo cha nguvu kazi chini ya daraja ukitoa usimamishaji wa nguzo kuu, deck zote hutengenezwa juu kwa juu baada tu ya kazi ya usimamishaji nguzo kukamilika.
Yana uwezo mkubwa zaidi wa kuhimili matetemeko ya ardhi ukilinganisha na aina nyingine za madaraja
Linaweza kubadilishwa kulingana na mahitaji, kama kubadilisha deck ili kukidhi mahitaji ya foleni.
Tucheki picha za Daraja hilo lililopewa jina la Nyerere Bridge