Mapigano ya wakulima na wafugaji yaliyotokea Alhamisi na kusababisha watu wanne kujeruhiwa katika Kijiji cha Makurunge wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani yamesababisha wilaya hiyo kuja na mkakati wa kuhakiki upya mifugo.
Uamuzi huo umetolewa na Baraza la Madiwani wilayani Bagamoyo baada ya kubaini kuwa bado kuna tatizo la kutoheshimiana kati ya wakulima na jamii ya wafugaji wilayani humo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Ally Issa alisema kuna haja ya kuangaliwa upya uingiaji wa wafugaji hao kama ni halali au ni wavamizi tu ndiyo maana hawafuati matumizi bora ya ardhi waliyojiwekea.