Basi linalotembea majini na nchi kavu lazinduliwa China | KINGAZI BLOG

KARIBU UHABARIKE KIGANJANI MWAKO.

Breaking News
Loading...

Wednesday, August 03, 2016

Basi linalotembea majini na nchi kavu lazinduliwa China

 Amini usiamini hili ni basi la kipekee linaloruhusu magari kupitia chini yake

Basi la kipekee lenye urefu wa mita mbili juu linaloruhusu magari ya kibinafsi kupitia mvunguni mwake limefanyiwa majaribio katika mji waHebei kaskazini mwa Uchina.

Basi hilo linalopigiwa upatu kutatua kabisa tatizo la usafirishaji wa watu katika miji yenye idadi kubwa ya watu ama Transit Elevated Bus (TEB) limefanyiwa majaribio nchini China.

Basi hilo linaloendeshwa kwa umeme linauwezo wa kubeba zaidi ya watu 300 .

Basi hilo kubwa lina urefu wa mita 21 na upana wa futi 25 .

Hii ndio mara ya kwanza kwa wabunifu kuonesha basi hilo hadharani baada ya video yake kuvuja katika mitandao mwezi Mei.

 Ndani inanafasi kubwa mno inaweza hata kuwabeba abiria 300

 Basi moja la TEB linauwezo wa kubeba abiria wote katika mabasi 8 ya kawaida !

Majaribio ya basi hilo la kipekee yalifanyiwa katika barabara iliyofanyiwa ukarabati yenye urefu wa mita 300m.

Basi hilo linauwezo wa kuhudumu kwa kasi ya Kilomita 60 kwa kila saa.

Takriban mabasi hayo manne yanawezwa kuunganishwa na hivyo kuwa na dereva mmoja.

Hivi ndivyo inavyoonekana

''Mabasi haya ni ya kipekee na moja ya faida yake kuu ni uwezo wake wa kubeba abiria wengi sana 300 kwa kila basi, pia itaokoa sana nafasi barabarani'' alisema mhandisi mkuu katika mradi huo mpya wa usafiri Song Youzhou.

''Inahudumu kama vile treni za kisasa za umeme ila gharama ya kuwekeza kujenga njia na ukarabati barabarani ikiwemo ujenzi wa vituo maalum vya TEB ni 1/5 ''

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us