Rais
 JOHN POMBE MAGUFULI amekabidhi zawadi zenye jumla ya shilingi milioni 
tisa kwenye vituo ishirini na nne  vya watoto wa mitaani 
Kaimu
 Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii RABIKIRA MUSHI akizungumza na 
waandishi wa habari kabla ya kukabidhi zawadi za Pasaka zilizotolewa na 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh JOHN POMBE MAGUFULI
Rais JOHN POMBE MAGUFULI amekabidhi zawadi zenye jumla ya 
shilingi milioni tisa kwenye vituo ishirini na nne  vya watoto wa 
mitaani pamoja na wazee nchi nzima katika kuadhimisha sikukuu ya PASAKA.Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Kaimu Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii RABIKIRA MUSHI amesema kuwa zawadi hizo kutoka kwa raisi ni salamu zake kwa watoto wa mitaani wasiojiweza pamoja na wazee.
Naye mmoja wa wasimamizi wa kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani kilichopo MBURAHATI Sister INNOCENSIA KAGOMA na mmoja wa watoto wanaolelewa katika moja ya vituo vya kulea watoto cha MBWENI amemshukuru Rais MAGUFULI kwa zawadi hizo na kutoa wito kwa wadau wengine kuwa na moyo wa kusaidia watu wenye uhitaji