Hakuna jambo linalowasumbua
watu wengi katika uhusiano wa kimapenzi kama kumtambua mwenzi sahihi.
Upo msemo maarufu mitaani kwamba ni bora ukosee mambo mengine yote
lakini siyo
kukosea kumchagua mwenzi wa maisha yako! Swali la msingi,
utajuaje kama huyo unayeishi naye, awe mke, mume, mchumba au mpenzi ni
mtu sahihi?
Pengine nikuulize hata wewe msomaji wangu, unajuaje kama mwenzi wako
unayeishi naye au uliyenaye ni mtu sahihi kwako? Una uhakika gani kwamba
maisha yako ukiwa naye yatakuwa mazuri na hatakuja kuuvunja moyo wako?
Huenda wengi wakakosa majibu zaidi ya kuishia tu kusema: ni mtu sahihi
kwa sababu nampenda au ananipenda.
Hata hivyo, upendo pekee hautoshi kukufanya uamini kwamba huyo
uliyenaye ni mtu sahihi kwa sababu upendo kama zilivyo hisia nyingine,
kuna wakati huongezeka na kuna wakati hupungua au kuisha kabisa kwa hiyo
kama unampima mwenzi wako kwa kigezo hicho, ipo siku utahisi kwamba
pengine hukufanya uamuzi sahihi.
UTAMJUAJE KAMA NI SAHIHI?
Mtihani mkubwa ni namna ya kugundua kwamba huyo unayeishi naye ni chaguo
sahihi katika maisha yako. Yapo mambo mengi unayoweza kuyatumia kumpima
mwenzi wako lakini katika makala haya, tutazungumzia mambo manne ya
msingi.
UNARIDHIKA UKIWA NAYE?
Jambo kubwa na la msingi linaloweza kukuonesha kwamba upo na mtu sahihi
katika maisha yako ni kuridhika. Kuridhika ninakokuzungumzia hapa, ni
ile hali ya moyo wako kujihisi kama unapata kila unachokihitaji na huna
sababu ya kufikiria kuwa na mtu mwingine.
Kuridhika ninakomaanisha hapa, si lazima mtu awe na uwezo wa kukupa
magari, majumba au vitu vya thamani kubwa, hapana. Namaanisha ile hali
ya kuridhika kuanzia kihisia, kimawazo, kimapenzi na kimaisha kwa jumla.
Hujawahi kuona watu wanaishi maisha ya kimaskini lakini wana furaha,
wanapendana, wanaheshimiana na kudumu? Ni kwa sababu kila mmoja
ameridhika na mwenzake. Hujawahi pia kuona wake wa matajiri wanatoka
kimapenzi na mahausiboi au vijana wa mitaani? Ni kwa sababu
hawajaridhika kwenye maisha wanayoishi, hata kama wanapata kila kitu.
Wakati mwingine, baadhi ya watu hujaribu kufananisha uhusiano waliopo na
waliowahi kuishi nao (ex), si makosa kulinganisha lakini isiwe kwa
lengo la kubomoa.
Friday, March 25, 2016
Uliye naye ni mtu sahihi kwako au umebugi?
Published Under
MAKALA MUHIMU
About Author
BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi