Machangudoa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi.
WAREMBO waliokamatwa hivi karibuni kwenye msako wa machangudo na wazururaji uliofanywa na jeshi la polisi, wamefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Chamwino, mkoani hapa na kusomewa hukumu
.
Katika msako wa Machi 18, mwaka huu, warembo; Mariam Hamis (mkazi wa Mwembesongo), Shani Hassani (mkazi wa Mawenzi), Zawadi Shekilema (hakujulikana), Magdalena Joseph (mkazi wa Kihonda), Natasha Hassan (mkazi wa Kihonda), Wema John (mkazi wa Msamvu) na Happyness Pascal (mkazi wa Sabasaba) walikamatwa katika msako wa polisi maeneo ya Itigi.
Siku hiyohiyo, katika mtaa wa Kahumba, msako uliendelea ambapo warembo; Maria Thomas (mkazi wa Kahumba), Najma Shabani (mkazi wa Mafinga), Scola Petro (mkazi wa Sabasaba), Edna Joakim (mkazi wa Karume), Mwasiti Saidi (mkazi wa Boma Road), Aanita Saidi (mkazi wa Mawenzi), Nayma Rashid (mkazi wa Mlapakolo), Rehema Juma (mkazi wa Mafisa) na Leah Wesley walikamatwa.
Mara baada ya kukamatwa na upelelezi kukamilika, warembo hao walipandishwa katika mahakama hiyo ya Mwanzo chini ya Hakimu Jane Mella na kusomewa mashtaka yao kisha kutakiwa kujibu ndiyo au hapana.
Kuna baadhi walikiri kufanya kosa hilo kutokana na ugumu wa maisha ambapo waliokiri walihukumiwa kifungo cha nje kwa miezi minne huku wale waliosema hapana wakihukumiwa kifungo cha miezi minne au kulipa faini ya shilingi elfu hamsini kila mmoja.
Baadhi yao walifanikiwa kulipa faini hiyo, wengine walishindwa hivyo kujikuta wakitupwa gerezani kwenda kutumikia kifungo chao.