Kufuatia kukamilika kwa uchaguzi wa marudio visiwani ZANZIBAR , Katibu Mkuu wa Baraza la wawakilishi YAHAYA KHAMIS HAMAD
Katibu Mkuu wa Baraza la wawakilishi YAHAYA KHAMIS HAMAD
Akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani UNGUJA HAMAD ametoa ratiba ya kuanza kwa shughuli za baraza ikiwemo uchaguzi wa spika na kuwaapisha wajumbe wateule 76 wa baraza hilo katika siku hiyo ya kwanza, Siku ya pili ya kikao kutafanyika uchaguzi wa naibu spika na wenyeviti wa baraza.
Tarehe 5 mwezi april utafanyika uchaguzi wa wajumbe wa baraza na uchaguzi wa wajumbe 5 watakao ingia katika bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Tarehe 6 mwezi April kikao cha baraza kitaahirishwa rasmi.
Mpaka sasa mwanachama wa chama cha Mapinduzi ZUBERI ALI MAULID ndiye aliyechukua fomu ya kuwania nafasi ya Uspika wa baraza la wawakilishi