Rais
JOHN MAGUFULI amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii ili
kuharakisha maendeleo ya nchi na kukuza uchumi wa taifa ikiwa ni sehemu
ya kuondokana na umasikini nchini
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akisalimia waumini huku akisikilizwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya
Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania Dkt. Alex Malasusa na Mchungaji Chalres Mzinga baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016
Rais MAGUFULI amesema hayo Jijini DSM katika Ibada ya
PASAKA alipopata fursa ya kuwasalimu waumini wa Kanisa la Kiinjili la
Kirutheri AZANIA FRONT alipokwenda kusali pamoja na mkewe mama JANET
MAGUFULI.Tanzania Dkt. Alex Malasusa na Mchungaji Chalres Mzinga baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016
Pamoja na mambo mengine Rais MAGUFULI amesema kipindi hiki cha sikukuu watanzania wanapaswa kudumisha upendo na kujenga umoja kwa taifa zima ili kufikia malengo mbalimbali ya maendeleo.
Awali akitoa mahubiri katika ibada ya pasaka Askofu wa Kanisa la Kiinjili la kiluteri Tanzania Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dokta ALEX MALASUSA alisema wananchi wote wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu ili kuweza kushinda changamoto mbalimbali katika jamii ikiwemo rushwa.