Rais wa Ufaransa,
Francois Hollande, amesema kuwa kundi la Waislamu wenye itikadi kali
walioshambulia Ufaransa mwaka uliopita na mashambulizi ya juma
lililopita ya Brussels wanaendelea kuangamizwa.
Alisema Serikali za Ufaransa na Ubelgiji zimefaulu kupata wanakojificha wengi wa wapiganaji hao na kuwatia mbaroni.Hata hivyo, Rais Hollande, alisema kundi hilo bado ni tishio kwa wakaazi wa Ulaya.
Maafisa wa polisi wa Ubelgiji wamewapiga risasi na kuwajeruhi washukiwa wawili katika oparesheni ya hivi karibuni.
Picha za video zinaonyesha maafisa wa usalama waliojihami na kujifunika kikamilifu wakiwa wamemlenga mwanamume mmoja aliyekuwa amejeruhiwa kabla ya kumkokota kwa miguu yake.