MWANAMUZIKI Rihanna, amekasirishwa na kitendo cha ‘ex’ wake, Chris Brown kumfananisha na wanawake wengine aliowahi kutoka nao kimapenzi.
Hivi karibuni Chris alipost kwenye Instagram picha aliyoiunganisha ikimuonyesha akiwa na
wanawake wanne tofautitofauti akifurahi nao sehemu mbalimbali, mmojawao akiwa ni Rihanna, wengine walikuwa Karrueche Tran, Draya Michele na Jasmine Sanders.
“Hajapendezewa na kitendo cha kulinganishwa na wanawake wengine wa Chris, hasa huyu Karrueche,” alisema rafiki wa karibu wa Rihanna na kuendelea: “Hataki kumvunjia heshima mtu yeyote, lakini Riri ni zaidi ya wote hao. Kila sehemu yeye ataendelea kung’ara kama almasi na haitabadilika kuwa ni zaidi ya wanawake wote aliowahi kuwa nao Chris.”