Siku chache baada ya wakuu wa mikoa kuapishwa na Rais John Magufuli, 
imeelezwa kuwa wakuu hao wametoa agizo la kuhakiki taarifa za watumishi 
wa umma kwenye mikoa yao. 
Agizo hilo la Rais linalenga kubaini 
watumishi hewa katika mikoa na wilaya nchini. Kazi hiyo imeanza 
kutekelezwa kwenye baadhi ya hospitali za Serikali nchini. 
Taarifa
 zilizoptaikana jana, zimeleza kuwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke na 
nyingine za mikoani, watumishi wote wametakiwa kupeleka viambatanisho 
kadhaa kwa ajili ya uhakiki wa taarifa zao za ajira. 
Chanzo 
kutoka hospitali ya Temeke kilieleza kuwa viambatanishi hivyo ni pamoja 
na barua ya ajira, wasifu wa kazi na stakabadhi ya malipo ya mshahara. 
Chanzo
 hicho kilisema kuwa agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa 
wiki iliyopita na wafanyakazi wanatakiwa kukabidhi viambatanisho hivyo 
kuanzia wiki hii. 
Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Temeke, Joyce 
Msumba alisema, “Hatuhakiki watumishi wa sekta ya afya tu ni watumishi 
wote wa umma.” 
Alisema watumishi ambao wako nje ya vituo vyao vya kazi, wametakiwa kurejea mara moja kwa ajili ya kazi hiyo.